Al-Balad

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa Mji huu! لَا أُقْسِمُ بِهَذَا الْبَلَدِ
2 Nawe unaukaa Mji huu. وَأَنتَ حِلٌّ بِهَذَا الْبَلَدِ
3 Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ
4 Hakika tumemuumba mtu katika taabu. لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ
5 Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ
6 Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا
7 Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ
8 Kwani hatukumpa macho mawili? أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ
9 Na ulimi, na midomo miwili? وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ
10 Na tukambainishia zote njia mbili? وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ
11 Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ
12 Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ
13 Kumkomboa mtumwa; فَكُّ رَقَبَةٍ
14 Au kumlisha siku ya njaa أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ
15 Yatima aliye jamaa, يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ
16 Au masikini aliye vumbini. أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ
17 Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ
18 Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. أُوْلَئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ
19 Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ
20 Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ
;