Al-Fajr

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa alfajiri, وَالْفَجْرِ
2 Na kwa masiku kumi, وَلَيَالٍ عَشْرٍ
3 Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja, وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ
4 Na kwa usiku unapo pita, وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ
5 Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? هَلْ فِي ذَلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ
6 Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di? أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ
7 Wa Iram, wenye majumba marefu? إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ
8 Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ
9 Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni? وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ
10 Na Firauni mwenye vigingi? وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ
11 Ambao walifanya jeuri katika nchi? الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ
12 Wakakithirisha humo ufisadi? فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ
13 Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ
14 Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia. إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ
15 Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ
16 Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge! وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ
17 Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, كَلَّا بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ
18 Wala hamhimizani kulisha masikini; وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَى طَعَامِ الْمِسْكِينِ
19 Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا
20 Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا
21 Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا
22 Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, وَجَاء رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا
23 Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّى لَهُ الذِّكْرَى
24 Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu! يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي
25 Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ
26 Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ
27 Ewe nafsi iliyo tua! يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ
28 Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. ارْجِعِي إِلَى رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً
29 Basi ingia miongoni mwa waja wangu, فَادْخُلِي فِي عِبَادِي
30 Na ingia katika Pepo yangu. وَادْخُلِي جَنَّتِي
;